FIZI:ASKARI JESHI WA TAIFA FARDC WASHTUMIWA KUWA CHANZO CHA USALAMA MDOGO PA SANZA SEKTA YA TANGANYIKA.

Écrit par sur juillet 11, 2019

Ph/Enoch David

Yapata sasa wiki na nusu tangu kushuudiwa kwa vitendo vya unyanyasaji vinavyosadikika kuhendeshwa na askari jeshi wa taifa FARDC ndani ya kijiji cha Sanza Sekta ya Tanganyika tarafani Fizi.

Kiongozi moja wa kijiji hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe kwenye vyombo vya habari alihihambia Radio yako siku ya tatu 10 Julai 2019 kuwa anasikitishwa sana na hali hiyo ya askari Jeshi ya kuwa wakipokonya vitu vya raiya kama vile simu mida ya usiku, pesa na hata vitu vingine muhimu  » Vijana wanatembea barabarani wananyanganywa simu, wanapigwa bila kosa. Wanabomowa milango ya raiya wanahingiya ndani ya majumba wanachukuwa vitu wanavyotaka hadi kuna wakati wanafyatuwa risasi kiolela bila sababu yoyote. Kuna askari jeshi aliyehomba kijana mmoja pesa heti anunuwe pombe Yule kijana akamwambia kuwa hana hela Yule askari akahanza kumtishia maisha tutahishi hivyo mpaka lini ?_ » alihuliza Kiongozi huyo.

Hata hivyo amehongeza kuwa endapo viongozi wa kijeshi hawatobadili askari jeshi hao eneo hilo wakaaji wote watahama kijiji hicho na kuhachia askari jeshi kijiji.  » _Hivi kuna askari ambaye alifika sehemu fulani ambapo palikuwa kilio akahanza kuhomba pesa kwa vijana ambao walikuwa nacheza mchezo wa draft « Dame », wakati Vijana hao walimwambia kama hawana pesa askari huyo akanyanganya kibao cha draft na kuhanza kukivunja Jambo ambalo lilikuwa limeshazusha gasia kubwa kwa Vijana hao ila walitulizwa nasi. Kama hali hahitobadilika tutahacha kijiji wazi ili wabaki wenyewe » alimalizia kusema Kiongozi huyo.

Upande wa askari jeshi wamesema kutokuwa na ripoti yoyote Kuusu hali hiyo na kuhahidi kuhifuatilia kwa makini ili kubahini ukweli wa mambo.

Mwishowe tukumbushe kuwa inapofika saa moja usiku raiya wote huwa wanahitajika kubaki majumbani kwao kwa kuhofia usalama wao.

©Bahome Sadi François

http://www.fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *



En ce moment

Titre

Artiste

FiziMedia

GRATUIT
VOIR