FIZI-MINEMBWE : SHIRIKA LA RAIYA LATAJA KUWA WIZI WA NGOMBE NDIO KERO KUBWA INAYOBAKI KWA KUPATA AMANI YA KUDUMU
Écrit par FiziMediaCongo sur août 15, 2019

Ph/Radio Brk fm
Wakati wa mahojiano na idhaa yako juma tano hii 14 Agosti 2019, mwenyekiti wa shirika la raiya tawi la manispaa ya Minembwe Bwana WILLIAM ETABO WA ROGER amehonesha kuwa usalama umeshahimarika katika manispaa ya Minembwe na vitongojini mwake, ila tatizo kubwa limebaki la makundi yenye kushikilia silaha kinyume na sheria kuhendelea kuhiba mali za raiya hususani ngombe bila kujali mazara yatokanayo na wizi huo. http://www.fizimedia.com
Mwanzoni mwa wiki hii ngombe mia moja ndizo zilipelekwa na wezi hao licha ya zimoja zilizokuwa zimebebwa kurudishwa kupitia jitiada za askari jeshi wa taifa FARDC ambao walihendesha mapambano makali na makundi hayo wiki iliyopita na kupelekea wao kubahatika kurudisha ngombe mia na hamsini, Alihongeza WILLIAM.
Hata hivyo ngombe zingine ambazo hesabu yake bado kujulikana zimepelekwa na watu hao hao tangu mwanzoni mwa wiki tunayo ndani ya Kijiji cha Nakiele, sekta ya tanganyika tarafani Fizi, mazungumzo bado yanahendelea kwa kutafuta mbinu za kurudisha mifugo hiyo.
Tangu kusitishwa kwa vita vya ukabila katika maheneo hayo hali imebaki kuwa tata kutokana
na wizi huo ambao unahacha raiya kwenye sintofahamu na kutokujuwa wafanye nini ili mambo hayo yafike mwisho.
Fahamu kuwa hali ya usalama mdogo katika vijiji vingi vya nyanja za kati na za juu ilihanza kuripotiwa tangu mwanzoni mwa mwezi Mey 2019.
Vyanzo: rb
fizimedia.com