FIZI-BARAKA:HABARI ZETU ZA LEO, Nundu, Kabumbe, Bukavu, Itombwe-Minembwe, Bukavu, Kinshasa na Nyarugusu camp, Yalio jiri.

Écrit par sur septembre 11, 2019

Uwariri: radio RTO NUNDU

1.Nundu.

Septemba 9. 2019, ugawaji wa vyandaruwa yenye dawa umeanzishwa kote jimboni Kivu ya kusini ukiwemo mtaa wa afya ya Nundu ndani ya tarafa la Fizi.
Chumba cha uhariri cha redio Tanganyika, kimewaomba wakaaji wote wa jimbo la Kivu ya kusini na wale wa mtaa wa afya wa Nundu kwa upekee kutumia vizuri vyandaruwa hivyo.
Vyandaruwa inayogabulika sio nyavu za kuroa samaki wala kamba za kufunga upango bali ni kwa ajili ya kukinga jamii zidi ya ugonjwa wa Maleria.
Ifahamike ya kwamba Maleria ni mojawapo ya magonjwa ambayo yanahuwa sana barani afrika ipatikanayo chini ya jangwa la Sahara._

2.Kabumbe.

Wasafiri waliokuwa wakitoka Uvira kujielekeza upande wa Baraka wamejikuta wamehanguka mikononi mwa wezi 4 wenye kushikilia silaa huko wakivaa nguo za kijeshi za kupasuka pasuka kijijini ASHINGENI-KABUMBE mchana wa leo septemba 10 mida ya saa nne za mchana.
Habari tuliyopata kutoka kwa mtu aliyekumbana na waalifu hao, yasema pesa na simu za mkononi ndivyo vilivyo chukuliwa na wezi hao wa kutumia silaa.
Mda mchache baada ya tukio, waanga wa tukio walikutana na wanajeshi wawili wa jeshi la taifa kwenye umbali wa mita chache na eneo husika na hivyo kuwapa taarifa ya kusema wameporwa na wezi wa silaa wapo pale, ila awakupata msaada wowote kutoka kwa wana jeshi hao, pindi wezi hao walikuwa bado awajatoka eneo hilo.
Eneo hilo la ASHINGENI-KABUMBE linasifika kwa vitendo hivyo vya wizi wa kutumia silaa kuliko eneo nyingi za tambarare ya sekta ya Tanganyika tarafa la Fizi mkoani Kivu ya kusini na kupelekea sehemu hiyo kubatizwa jina la 17.
Ifaamike ya kwamba kitendo cha mwisho kama hicho kimeripotiwa huko Ekwena hiyo siku ya jumatatu septemba 09 pale wezi walipohiba na kufyatua risasi kazaa hewani na kupotelea pasipo julikana._

Itombwe-Minembwe.

Baada ya makabiliano ilitokea huko TÚLAMBO wiki iliyopita na kusababisha kifo cha kiongozi wa waasi wa NGUMINO ambaye alijulikana kwa jina la SEMAHURUNGWE, usiku wa septemba tariki 08.http://fizimedia.com
Waasi hao wa NGUMINO walisumbuwa raia wa jamii za wafuliro na wa Bembe wapatikanao kijijini Kalingi, matokeo watu 02 wamefariki na wengine sita kujeruliwa._
Hadi mda huhu, hali ya usalama bado ni tete kijijini hapo.
Habari za hivi punde zasema ya kwamba vijiji vya NKANGO, RINSANSE na PEPE vyawaka moto mda huhu._
Vijiji hivyo vinakaliwa na jamii ya Banyamulenge.

Bukavu.

Mlipuko wa moto wa zuka hi leo siku ya nne septemba 10 ndani ya kata ya NYAMUGO MAHENGE 2 ndani ya jiji la Bukavu.
Kwa mujibu wa walio shuhudia tukio, tayari nyumba zaidi ya kumi na tano zimekwisha teketezwa na moto ambao bado unashindwa kuzibitiwa.

Kinshasa.

Raisi wa DRC, Felix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO amewasili brazzaville nchini Jamuhuri ya Congo.
Raisi amekwenda nchini humo ili kushiriki kwenye mkutano wa uchumi wa bara la Afrika ambao utakutanisha viongozi wa nchi na wawekezaji wa Kiafrika kwa lengo la kuwekeza barani.
Tufaamishe ya kwamba raisi Félix anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Ubelgiji munamo tariki 17 hadi tariki 20 mwezi desemba na atapokelewa na mfalme Philippe wa Ubelgiji kwenye jumba la kifalme.

Nyarugusu.

Hatua ya kupiga marufuku marufuku masoko madogo madogo huko kambini Nyarugusu, wilayani KASULU mkoani KIGOMA nchini TANZANIA imeanza kutekelezwa hiyo jana siku ya juma tatu septemba 10.
Ayo yalitokana na amri ya fois ya mkuu wa kambi ilio tangazwa siku ya juma pili septemba 8 ikisema ya kwamba: « Kuanzia juma tatu septemba 9 ni marufuku mkimbizi heyote yule kuonekana ndani ya masoko madogo madogo wala kasoko kwa kiswahili kingine akitereka bidhaa yoyote ile na atakaye kaidi na kushikwa atafikishwa mahakamani._

Michezo.

Timu ya soccer ya ETBS kutoka Sangya kutoka ndani ya sekta ya Tanganyika tarafani Fizi yapokea kichapo cha kike zidi ya timu ya FC KAMANYOLA ya huko Kamanyola tarafani Walungu pale walipo kubali kuchapwa mabao 4 kwa yahi (0) kwenye mechi iliyopigwa huko Kamanyola mwishoni mwa wiki hii.

Picha:http://www.fizimedia.com

©Enoch David.


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *



En ce moment

Titre

Artiste

FiziMedia

GRATUIT
VOIR