FIZI-HABARI ZETU:Mukolwe, Ekwena,Itota, Bwegera, Minembwe na Nyarugusu, yalio jiri.

Écrit par sur septembre 9, 2019

Uwariri wa radio RTEO NUNDU.

Picha:http://www.fiziledia.com na Enoch David.

1.Mukolwe.

Watu wasio julikana wenye kushikilia silaa wamehingia nyumbani mwa ANDRE mkaaji wa Mukolwe, grupementi ya Basimunyaka ya kaskazini sekta ya Tanganyika hiyo siku ya juma pili septemba 08 na kufanyikiwa kupora dolla 500, 350 000FC pamoja na mavazi. Kitendo hicho kimefanyika usiku.
Ikumbuswe kwamba hali ya wizi wa kutumia silaa pia uliripotiwa siku ya juma tano kijijini MINOVA/UP ndani ya grupementi ya Babungwe wa kaskazini pale kijana DEMULE aliporwa baiskeli, simu ya mkononi pamoja na elfu sabini pesa za Congo.

2.Ekwena/Baraka.

Waendesha piki piki pamoja na abiria wao wameporwa asubuhi ya leo Septemba 09. na watu waliokuwa na silaa huko wakivalia sare za kijeshi kijijini EKWENA kijiji kipatikanacho kwenye umbali wa kilomita 9 kaskazini mwa jiji la Baraka.
Kiwango cha kutosha cha pesa, simu 4 za mkononi ni miongoni mwa vitu vilivyo bebwa na wezi hao.
Kabla wenyewe kutimkia upande wa chini ya barabara wezi hao walifyatua risasi kazaa hewani kwa ajili ya kujichukulia usalama.
Mda mchache baadae jeshi la taifa (FARDC) kutoka Abela walifika eneo la tukio kwa ajili ya kuwatafuta waalifu ila awakufanikiwa kuwateka.
Tukio hilo limetokea pembezoni mwa kilalo cha mto MKYEMKYE upande wa EKWENA.

3.Itota.

Maiti moja yenye kuharibika zaidi iliokotwa porini kijijini Itota, kijiji kipatikanacho ndani ya sekta ya Mutambala.
Baada ya ukaguzi, imebahinishwa ni masalio ya mwili wa ASSUMANI KALUKULA ETUKU mzawa wa kijiji hicho, wa jamaa la Balala mwenye umri wa miaka 47.
Chanzo cha habari chatujuza ya kwamba mtu huyo alipotea tangu mwezi machi mwaka huhu.
Mifupa, nguo pamoja na viatu vya gaudiot vimezikwa kijijini hapo iyo jumapili ya septemba 08 mida ya alhasiri.
Ikumbukwe ya kwamba mahiti ingine ya mtu aliye julikana kwa jina la MSHINGI LUBYULA ALFANI iliokotwa kijijini Kichula wiki iliopita baada ya hali ya kutokuelewana yeye na mkewe.

Bwegera/Uvira.

Mtu moja aliyekuwa akitekeleza wizi wa kutumia silaa ameshikwa na silaa yake alipokuwa akivizia gari la hospitali ya Lemera iliyokuwa ikitoka Uvira kujielekeza Lemera.
Kwa upande wake bwana Willy SEREMBA mratibu wa shirika la raia nchini DRC aliyesibitisha habari hizo kunako media Congo.net amesema ulikuwa ni mda wa saa mbili ndipo mualifu huyo alitekwa nyara kati ya Bwegera na Nyamutiti eneo linaloitwa Kulibwe.
Gari hiyo imehingia nyara ndipo dereva na waliokuwemo ndani walijitolea na kufanikiwa kumdhibiti na kumfunga kamba na kumnyanganya silaa mwizi huyo na kumpeleka kwenye jeshi la taifa.
Mwizi huyo amesadikika kuwa moja wapo wa kundi la wanamgambo wa Buhirwa Asifiwe Kampa Mapera.
Habari hiyo imesibitishwa na msemaji wa jeshi la taifa ya operesheni ya Sokola kusini ya Kivu ya kusini, kapteni Dieudonné KASEREKA.

4.Minembwe.

Kanali aliyejitangaza SEMAHURUNGWE, kiongozi wa kundi la kijeshi la NGUMINO, afariki baada ya kupata majeraha kwenye mapambano makali yaliyo pambanisha kundi lake la NGUMINO na lile la MAÏ MAÏ ndani ya kijiji cha Túlambo, grupementi ya Basimukinji sekta ya Itombwe tarafa la Mwenga mkoani Kivu ya kusini.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la taifa huko MINEMBWE ambaye ametoa taarifa hizi amesema pia wa MAÏ MAÏ wawili walifariki kwenye pambano hilo na nyumba nyingi kuharibiwa.
SEMAHURUNGWE amefia njiani wakati alipokuwa akipelekwa kwenye hospitali ya Minembwe center kwa ajili ya matibabu zaidi.
Kwa mujibu wa habari za mahali zasema habari ya kuwepo kwa ayati SEMAHURUNGWE kijijini Túlambo zilijulikana mbele ya kuanza kwa mashambulizi ya juma mosi.

5.Nyarugusu.

Habari kutoka huko Nyarugusu zasema ya kwamba soko zote za wakimbizi zimefungwa kwa mda usio julikana._
Hiyo imetokana na na agizo lililo sahiniwa na mkuu wa makazi kambini hapo.

http://www.fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *



En ce moment

Titre

Artiste

FiziMedia

GRATUIT
VOIR