Fizi: vizuhizi vya hondolewa bara barani.
Écrit par FiziMediaCongo sur septembre 14, 2019
Madiba Maoye

Wabunge wajimboni Kivu kusini wachaguliwa wa tarafa ni Fizi,ijumaa tare 13 Septemba waendesha operesheni « safisha barabara » kwa kuondowa viziwizi kwenye barabara ya taïfa ya namba tano ambavyo ni kero kwa wasafiri wa kutoka Uvira na kujielekeza sehemu mbali mbali za tarafani Fizi.
Viziwizi hivyo vimekuwa vikilalamikiwa na mashirika ya kiraïa myaka nenda rudi bila kupatiwa ufumbuzi.
Viziwizi hivyo ni pamoja na maasifa wa serikali ambao hufunguwa ofisi ndogo ndogo kwenye daraja la mto Makobola unao gawa tarafa la Uvira na Fizi.
Eneo hilo idara itakayo Salia hapo ile ya Foner na polisi wa usalama barabarani,kwa mujibu kwa mujibu wa wanabunge hao.
Kutoka Makobola hadi kufika Nyange hakuna tena kiziwizi kitakacho onekana njiani. Wabunge hao wa jimbo wa chaguliwa wa Fizi wamejulisha.http://www.fizimedia.com
Asubuhi ya ijumaa hii tariki 13 /09/2019 kumengolewa kiziwizi ambacho kilikuwa kimesalia kijijini Malinde,ambako vitu kadha vimekuwa kwenye ofisi ya kwenye barabara kuu ya hapo kijijini Malinde ambamwo wafanya kazi wakutoza pesa za malipo ya barabara walikuwa wakitumikia emo,ni pamoja na pombe aïna ya gango,unga wa mahindi vyungu na tandiko. Katika Sakata hilo kiongozi wa Transcom tarafani Fizi akijulikana kwa jina la Kibaba,amewekwa kizuhizini kunako ofisi ya polisi ya taïfa district ya Fizi yenye makao yake mjini Baraka kwa muda wa masaa kadha kwa kupinga hatuwa hiyo ya wanabunge ya kuondowa viziwizi barabarani.