Nyarugusu camp:Akuna la mtu yeyote kuteraka kwa kuhuza au kununuwa vitu katika Masoko madogo madogo.
Écrit par FiziMediaCongo sur septembre 9, 2019
Raymond Misa miranam isaiah.

Photo :Babondommebalo
Ayo yalitokeya kutokana na amri kutoka ofisi ya mkuu wa kambi ilio tangazwa Jana Ijumapili 8 september, ukisema kwamba : kuanzia leo ijumatatu ya tarehe 09/ 09 /2019 asionekane mkimbizi yeyote katika Masoko madogo madogo akitereka bidhaa yoyote ile na atakae shikwa atapelekwa mahakamani.
Amri iyo kutoka MHA imehitikiwa kwa asilimiya tisini na tisa mkato tisa na wakimbizi wote iwe upande wa warudi aidha upande wa wakongomani.
Akuna mtu alie tereka kitu chochote kile sokoni leo wala kununuwa.
Kila soko ndogo lilikuwemo Masungusungu takribani wane asubuhi kwa lengo la kuzuia wafanya biashara wadogo wadogo kutolema.
Kwa nini Ayo yametokeya na wakimbizi wana maoni gani katika ili ?
Ripota wetu alijaribu kuhojiana na baadhi ya watu alio wakuta pembezuni mwa soko ndogo la E3 na lile la D1 katika kambi ya wakimbizi wa kikongomani na kumueleza yafuatayo:
» Sisi tumestushwa sana na amri iyi ya kutuzuhiya tusitereke vitu vyetu sokoni,
Mimi nahuzaga dagaa wa Mwanza,
Sijuwi kwa nini nisitereke sokoni,
Watu wengi wamekuja hapa sokoni kutafuta angalau wanunuwe viungo mbalimbali vya mboga, unga, mchele na kazalika lakini wanaangaika atujuwi kwa nini » alisema mama Nyassa, muhuza dagaa wa Mwanza katika soko ndogo la E3.
Nae Andréa Idi alikuwa na aya yakusema:
» soko ndogo na kubwa zote zimefungwa, watu wengi hawajuwi kwa nini ila mimi nazani ayo yametokeya kwa lengo la kuwashinikiza warundi waandikwe ili warudi kwao.
Kwa kuwa mimi naona kwa maana warundi hawaandikwi tena kwa hiari kurudi kwao, basi viongozi wa nchi wameona wakitufungiya activity za kibiashara basi warundi wataandikwa kwa wingi kurudi kwa hiari »
Je, baadhi ya wakuu viongozi wa Masoko madogo ayo walisema nini?
Tulijaribu kuojiana na kiongozi wa soko ndogo la E3, Angùla , yeye alisema kuwa » Niliongeya na viongozi walio juu yangu kutaka kujuwa sababu za soko zetu kufungwa ila alinijibu kuwa atatujulisha baadae na sio leo, niwe na subira katika ili na niwaambiye wenzangu wasileme sokoni mpaka pale tutakapo ruhusiwa.
Ifaamike kwamba maswala ya wakimbizi kufungiwa wasifanye biashara na mengineyo sio geni kambini nyarugusu.
Na ni takribani mwaka mzima sasa toka soko kuu la Muungano lifungwe mnamo Agosti 15, 2018.
Pia usafili wa Pikipiki na besikeli ulifungwa ingawa viongozi wa kambi waliyetelea sana kuwa wafunguliwe usafiri wa besikeli kwa kuwa ni msaada kwa wakimbizi kusomba chakula wanacho kipokea store kutoka WFP.
Na serikali ikahamuwa kufunguwa besikeli kutembelewa kambini nyarugusu ingawa Pikipiki zilienda mazima.