Mahafa ya Mafuriko inchini Kongo: Ujumbe wa Serikali na ule wa ikulu ya Raïs Félix-AntoineTshisekedi wa maliza ziara yao
Écrit par FiziMediaCongo sur mai 5, 2020

Ujumbe wa Serikali ya Jamuhuri ya kidemokratiya ya Kongo na ule wa ikulu ya Raïs ume maliza ziara yao ya kikazi katika tarafa ya Malemba Nkulu katika Mkowa wa Haut-Katanga kisha kutembeleya miji kama, kindu,Goma,Bukavu,Uvira,Kalemie,Moba, Manono na kamina mashariki mwa inchi hiyo.
Ziara hiyo ililenga kutasmini maafa ya mafuriko iliyo sababishwa na nvua kali iliyo nyesha mwezi wa inne uliyo pita ambapo kuliripotiwa matokeo ya watu kufariki, vitu kaharibika na nyumba kubomaka.

Jean-Jeacques ELAKANO, mshauri wa rais wa DRC Felix TSHISEKEDI akiwa ndani ya msafara huo amesema amesema ziara yao maeneo hayo imezaa matunda.
Wakiwa katika jiji la Lubumbashi wakisubiri safari ya Kurejeya Kinshasa, Mwana sheriya Jean Jacques Elakano, aliweza kukubali Mwito wake mwana Bunge wa Taifa Maeneo hayo Bwana Fabien Mutombe Kankanto wa chama chenye kuwa madarakani inchini Kongo, UDPS huku wakisindikizwa na wana memba wengine wa chama hicho kwa kuhimiza wakaaji wa manispa 5 za jiji la Lubumbashi kwa hatuwa ya kujinga na ugondjwa wa Coronavirus ambao unahatarisha taifa hilo, amesema Jean-Jeacques ELAKANO.

Viongozi hao waligawa maski za kujikinga zidi ya ugondjwa huo, jambo ambalo raiya wa Lubumbashi wame pongeza kwani wengi awaku tarajiya hayo kutokea.
Mwana Bunge Fabien Mutombe Kankanto aliweza pia kumpeleka mbunge wa taifa mchaguliwa wa tarafa la Fizi, Msambya Abwe Freddy na Jean Jacques Elakano kunako ofisi ya chama hicho katika jiji hilo la Lubumbashi.

Mbunge huyo wa taifa Fabien Mutombe Kankanto aliweza kumvalisha Jean Jacques Elakano Kitambaa cha chama hicho kama ishara ya msimamo wake katika chama na kuongoza chama icho kwa muda wa Miaka 11 bila kugeuza msimamo wake.
kwa kipindi cha miaka hiyo 11 aliweza kupitisha wabunge pia, alivalisha Msambya Abwe Freddy Kitambaa kwa kuchaguliwa kama Mbunge.

Jean Jacques Elakano alipongeza hatuwa iyo ya chama chao cha UDPS kwa hatuwa hiyo.
Hadi sasa msafara wa serikali ya Kongo na hule wa ikulu ya Raïs Félix-Antoine Tshisekedi una jihandaa kurudi Kinshasa ilikutowa ripoti ya kazi walio pewa ivi karibuni.
Licha ya mafuriko hayo Inchi ya jamuhuri ya kidemokratiya ya congo DRC, inakuwa ikipitiya katika kipindi kigumu wakati huu, Uwepo wa ugondjwa wa Covid-19, mripuko wa homa kali ya Ebola mara tena Wilayani Beni mashariki mwa inchi hiyo na Mahuwaji ya raiya yanayo endeshwa na wahasi wa ADF.

Raïs wa inchi hiyo, Mh. Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo anajitaidi kubadili Mfumo wa uwongozi wa inchi iyo baada ya Raïs Mstafu Joseph Kabila Kuachiya madaraka mwaka wa 2018 ulio pita.
– Uwariri wa FiziMedia.