Fizi :  » Kanali Makanika Haja fariki , yupo hai, Habari zilizoko mitandaoni ni za uzushi Mtupu » Gadi Mukiza Sabimana

Écrit par sur juin 6, 2020

Akizungumza na vyombo vya habari vya jiji la Baraka, mnyapara wa manispaa ya Minembwe Bwana GADI MUKIZA SABIMANA, amehakikisha kuwa hakuna ukweli wowote unahohuusu kifo cha mkuu kiongozi wa kundi la wahasi wanahohendesha mapambano katika vijiji mbali mbali vya nyanja za juu Bwana MAKANIKA RUKUNDA.

Mnyapara huyo amesema kuwa MAKANIKA yuko hai, na habari zote zilizovumishwa kwenye mitandao ya kijamii na hata baadhi ya vyombo vya habari si kweli na ni uzushi mtupu.

Aidha amehongeza kuwa, hali ya usalama ndani ya manispaa yake si yenye kurizisha kwani vijiji vingi vyenye kuwa pembezuni mwa manispaa hiyo vinazidi kugeuzwa kuwa shamba za mapigano kati ya mai mai na kundi la ngumino wakishirikiana na kikundi chake makanika.

Makanika alikuwa afisa wa juu wa Jeshi nchini DRC mwenye cheo cha Kanali ambaye alihihasi Jeshi na kuhunda kikundi chake cha uhasi nyanja za juu.

Bahome Sadi Fr.


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *



En ce moment

Titre

Artiste

FiziMedia

GRATUIT
VOIR