Fizi: wana mgambo wa tano wa Makundi yenye kumiliki silaa wa kamatwa mateka na jeshia la taifa huko Mboko
Écrit par FiziMediaCongo sur juin 6, 2020

Jeshi la taifa FARDC limetaja kukamata mateka 5 wa muhungano wa makundi yenye kumiliki silaa kinyume cha sheria wakihongozwa naye afisa wa Jeshi hilo aliyehasi Bwana MAKANIKA.
Ni wakati Jeshi liliweka mtego [Ambuscade] ndipo walibahatika kuwakamata, huku wakiwa na silaa 2 AK47, Gurumeti 1 na risasi 350 kijijini Mboko sekta ya Tanganyika tarafani Fizi.
Msemaji wa Operesheni ya Kijeshi Sokola 2 kusini mwa Jimbo la Kivu kusini, Kepteni Dieudonne KASEREKA, amehongeza kuwa mapambano makali yanahendelea kwenye nyanja za juu kati ya kijiji cha Mulima na Minembwe kati ambako Jeshi lilibahatika kufunguwa njia iliyokuwa imefungwa na wanamgambo hao wakihongozwa na Makanika.
Wanasiasa nchini DRC wamehomba Jeshi kufanya kila jitiada ili kuhakikisha Makundi yote hayo yanateketezwa na kuweka silaa chini huku wakikazia swala la kuhongeza idadi ya askari Jeshi kwenye maheneo hayo ya nyanja za juu.
– Bahome Sadi Fr.