FIZI: mama mmoja ahuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasio julikana Kijijini Abwalé.
Écrit par FiziMedia sur juin 27, 2022
Kwa muhujibu wa shirika la Raia chunvi ya Congo tarafani Fizi,kupitiya msemaji wake ,Nebo Mboka, mama huyo ajulikana kwa jina la NA’ÙMBÙ mwenye umri wa miaka 70, mkaaji wa Kijiji cha Abwalé ndani ya groupement ya Bashi Loca ,sekta ya Tanganyika tarafani Fizi alipigwa risasi na watu wasio julikana usiku wa kuamkiya Siku ya Inga tarehe 26/06/2022.
Uongozi wa shirika hilo la Raia, unakemeya vikali vitendo ivyo ambavyo vinajizihirisha Siku baada ya Siku ndani ya tarafa la Fizi.
Huku ikumbushwe kwamba kitendo kingine cha ukatali kama n’a hicho kwa Siku hizi, ni kile kilichokeya Kijijini BÙKÙ ndani ya sekta ya Tanganyika ,ambako mama mwengine mwenye kukadiriwa kuwa n’a miaka zaidi ya 50, ambaye alihuwawa piya kwa kama na hiyo usiku wa Siku ya pili tarehe 21/06/2022.
fizimedia.com