Fizi: mama mmoja na mwanaye wahuwawa kwa kupigwa risasi Kijijini Lweba.

Écrit par sur décembre 5, 2022

Mama pamoja na mwanaye wapoteza maisha kwa kupigwa risasi Kijijini Lweba, groupement ya Bashi m’nyaka kaskazini,sekta ya Tanganyika usiku wa Siku ya nne tarehe 01/12/2022.

Kwa mujibu wa shirika la Raia Kijijini hapo, watu wenye kushikiliya silaa waliingiya ndani ya nyumba ya mama huyo mida ya saa Tano usiku(23h).

Mama anajulikana kwa jina la Nyassa Ebinda mwenye umri wa miaka 62 ,mkaaji wa Lweba ya kwanza,ambaye alipigwa risasi pamoja na mwanaye kwa jina Paul Maandiko mwenye umri wa miaka 14ans na kufariki papo hapo.

Na mtoto mwengine ajulikanaye kwa jina la Ngyebwa Maandiko mwenye umri wa miaka 17, alijeruliwa vikali.

Chanzo cha kitendo hicho Bado kujulikana ,ila yawezekana tuhuma za kichawi kuwa miongoni mwa kitendo ,kama zilivyo heleza duru zingine.

Shirika la Raia,limelaani kitendo hicho cha ugaidi na limeomba vitengo husika kuwajibika na uchunguzi ili kubaini wahalifu.

fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *



En ce moment

Titre

Artiste

FiziMedia

GRATUIT
VOIR