FIZI-RDC : Mshauri wa rais wa DRC, ahusikaye na Sanaa pia na Dini amesema ahata wasili tarafani fizi mwishoni mwa mwezi huu kwa sababu ya kushiriki kwenye mazishi
Écrit par FiziMedia sur mai 29, 2019
Mshauri wa rais wa DRC, ahusikaye na Sanaa pia na Dini amesema ahata wasili tarafani fizi mwishoni mwa mwezi huu kwa sababu ya kushiriki kwenye mazishi ya mwili wa aliye kuwa kiongozi wa upinzani inchini humo aliye fariki february 2017, jijini Bruxelle inchini ubeljiji.
Jean-jeacques ELAKANO, mchauri huyo amezibitisha kuwa ziara yake tarafani fizi ya kuja kutasmini mpango wa siku miya moja wa raïs Félix Tshisekedi, imehahirishwa kwa sababu ya kurejeshwa kwa mwili wa aliye kuwa kiongozi wa upinzani, Étienne TSHISEKEDI WA MULUMBA.
« Familiya ya ayati mkongwe wa siasa hapa inchini Étienne tshisekedi imesema mwili wa mkongwe huyo utawasili hapa inchini DRC May 30 na kuzikwa tarehe moja juni mwaka huu, habari hiyo Ndiyo imehahirisha ziara yangu » ametaja Jean-jeacques ELAKANO.
Pia ameongeza kwamba siku hiyo itakuwa siku ya historiya hapa inchini, Étienne TSHISEKEDI ni mfanya siasa ambaye alipiganiya inchi hiyi kwa kuwa na democratiya.
Étienne TSHISEKEDI ni baba wa raïs wa sasa Félix TSHISEKEDI.
Mwili wa Étienne TSHISEKEDI umekaa ubeljiji tangu february 2017 baada ya kuzuka utata kati ya serkali ya DRC zidi ya chama chake cha udps.
Uhongozi wa chama ulitaka azikwe kwenye makao makuu ya chama hicho mjini Kinshasa, swala ambalo serkali ilikataa wakati ikiongozwa na raïs mstafu Joseph Kabila, amemaliziya kusema Jean-Jacques ELAKANO.
Masuku kashindi
Www.fizimedia.com