MISISI: Fizimedia.com ya towa ukweli kidogo kuhusu hali ya usalama katika mji wa Misisi jimboni kivu ya Kusini baada ya Utafiti
Écrit par FiziMedia sur mai 29, 2019
MISISI:
Fizimedia.com
ya towa ukweli kidogo kuhusu hali ya usalama katika mji wa Misisi jimboni kivu ya Kusini baada ya Utafiti
Sasa imepita Wakaaji wa Misisi wanaangaika na kukoseshwa Amani, huku kazi zao kuaribika, kunyanyaswa, kunyanganywa Mali zao na kupigwa Risasi kiholela na jeshi la jamuhuri ya kidemokratia ya kongo FARDC kando la kitengo cha Bana Mura, ndani ya mji wa Misisi, katika secta ya Nganja, tarafani Fizi mu jimboni kivu ya kusini
Hali ambayo inakuwa inawasumbuwa raiya wengi wakati huu.
Kulingana na shirika la raiya maeneo yaho, limesema kuwa,kitengo cha jeshi cha Bana Mura cha jeshi la taifa FARDC kinakuwa kinaweka hofu nyingi ndani ya wakaaji na mpaka sasa kinaonekana kuwa chanzo cha ukosefu wa usalama ndani ya muji wa Misisi.
Vurugu na fujo zilianza tarehe 19. Mai, pale ambapo vikosi vya jeshi la taifa vilipo panda milimani na kwenda kupiga na kufukuza jeshi la wahasi wa MAI MAI wake General AMULI maharufu YAKUTUMBA ambao kwa wakati huo Walikuwa Wanamiliki kilima cha Uchimbaji madini cha kachanga.
Raiya wengi wa secta ya NGANJA walionekana wenye furaha wakati uhusihano mzuri wa wahasi wa MAI MAI na jeshi la taifa FARDC huku wakizani kuwa labda ndiyo mwisho wa uhasi maeneo yaho kama alivyoahidi mweshimiwa Raisi wa jamuhuri ya kidemokrasiya ya kongo FELIX ANTOINE Tshisekedi.
Hali inakuwa mbaya mno wakati pale vikosi vya jeshi FARDC vilianza piga risasi ovyo ovyo na Makombora,wachimbaji madini wakakimbia vikosi vya jeshi vakaanza kuiba Mawe ya dhahabu na Mali zingine za raiya hao, wakati huo Mai Mai walikaa kimya hawakujibu chochote.
Tangu hapo hali zilianza kuwa ngumu upande wa raia, waaskari walifanya maovu mengi kwa kusingizia kila raiya kuwa ni MAI MAI, watu walinyanganywa simu zao, pesa mchana kutwa tena hazarani bila aibu, uki pinga unapigwa risasi, hali hiyo ilitusikitisha sisi kama kinwa cha raiya [Shirika la raiya la maeneo hayo].
Mda mchache tu ,vikosi vya MAI MAI vili hamuwa kuhama na kutoka maeneo ya KACHANGA na kuanza kuvuka Maeneo ya Lubichako ambako FARDC walianza kuwazuia na kuwatupia risasi,hadi hapo vikosi vya wahasi MAI MAI waliamuwa kujibu vita hivyo, Ushaidi wa www.fizimedia.com ulihakisha kuwa, takribani askari 13 wa jeshi la taifa FARDC walipoteza maisha katika makabiliano hayo,pia na raiya 2 waliripotiwa kufariki.
Shirika la raiya la huku lilisema kuwa, wa hasi hao wa MAI MAI Wali weze kuzibiti Kijiji icho cha KACHEMBA kwa muda wa takribani saa 7 Mpaka usiku wakaondoka zao na kupanda Milimani.
Bahada ya siku mbili,tangazo liliwekwa wazi huku likiomba wachimbaji madini kuweza kurudi mashimoni na kuhendesha kazi zao kama kawaida,lakini jeshi liliomba kila mtu aweze kuwa na kadi yake ya uraiya, hivo kazi zilianza ila usiku ndani ya doria,vikosi vya jeshi vilianza ogopa kuvamiwa na wahasi na kuanza kupigana risasi wao kwa wao wakizani ku ni maadui,asubuhi mda mchache ushaidi ulionyesha kuwa askari wawili walifariki pamoja na raia mmoja aliyeshikwa na risasi wakati alipo kuwa akitokea kunako kilio usiku.
Asibuhi yake walipo kuwa wapeleka maiti hizo za askari mbili kunako hospitali kuu ya Lulimba nilikuwa kunako korti, hapo pia tulisikia Milio mingi ya risasi kunako soko kuu ya MISISI, Wana jeshi walifika kunako soko,waka chukuwa dodoma 2,hali hiyo ilikuwa yenye kuvutisha machozi mengi wakati hule kanali wa jeshi alikuweko wakati jeshi lina nyanyasa raiya azarani.
Baada ya siku chache tangazo ikawekwa na shirika la wachimbaji madini la COOMIKI kuwawajimba migodi wote washuke manyumbani huku jeshi la taifa FARDC linataka hanzisha opération ya siku ine zidi ya wahasi wa MAI MAI.
Kusema kweli,hali ya Misisi ilikuwa mbaya wakati huu, raiya wanakuwa wakichimba madini kuanziya saa moja hadi saa sita mchana,lakini siku chache vikosi vya jeshi FARDC,kitengo cha WANA MURA kilipata oda kutoka kwa viongozi wao ilikuweza kuondoka maeneo hayona kuachiya vikosi vivya vya FARDC aina ya ZOLO ZOLO ambavyo hadi sasa raiya wengi wa Misisi wanasema kuwa ni wana jeshi wa kabila la Wahuti,na watutsi ambao wanachangana na wakongomani alisi[ fizimedia.com].
Ilipo fika mida saa mbili ya asubuhi siku ya ine,tarehe 25/05/2019, wachimba madini wengi walishuka kutoka milimani huku wakisema kuwa wamechoshwa na tabia mbaya ya Jeshi ya kusema kuwa kila mchimbaji madini eti ni MAI MAI,hali hiyo,ilileta woga sana na ivo tena milio mingi ya risasi ilisikika kuanzia mapema hadi mida ya jioni.
Wana harakati wengi wa haki za binadamu tarafani Fizi tunajihuliza ni lini haki ya raiya itaweza kuheshimiwa umu ichini jamuhuri ya kidemokratiya ya kongo wakati huu raiya wengi wa tarafa hilo wanapendelea hata kutumika na jeshi la waasi wa MAI MAI kuliko jeshi la taifa.
Hivo hadi sasa askari jeshi wa taifa wanakuwa wakilipisha wachimabji migodi pesa 1000 FC kabla ya kupanda kunako kilima ili kuchimba madini.
Raiya wa muji wa MISISI wanaomba wachaguliwa wao ki ubunge hna rais wa jamuhuri ya kidemokratiya ya kongo kuweza kuchukuliya swala la ulinzi wa raiya na mali zake ili liweze kupata suluhisho.
Habari hizi tunahendelea kuzifuatilia kwa ukarimu na kuwapa yote iliyo jiri.
fizimedia.com
Mwandishi na Mtafiti : Enoch David