http://www.fizimedia.com Uvira:Mji wa uvira wavuma kwa shindo, Jean Jacques Elakano ndani ya Mkutano na raiya Leo Jioni
Écrit par FiziMediaCongo sur juin 24, 2019
David Aluta

Mamiya na ma elfu ya raiya wa muji wa uvira wamefurika asubui hii wakichunga kunako kilalo cha Kavinvira kuwasili kwa msafara mkubwa wa raisi wa inchi Felix Tshisekedi Ambao unahongozwa naye Mweshimiwa naye Mshauri wake Mwanasheria Jean Jacques Elakano.
Jean Jacques Elakano amesema kuwa, « Imekuwa siku nyingi aongoye, lakini Leo nitaongeya na raiya wa muji wa Uvira kupitia Meeting ,ili nijuwe matatizo ya raiya wa muji wa Uvira »Ndivyo alisema huyo wakati Wa Maojiano ya pamoja na www.fizimedia.com.
Jean Jacques Elakano kwengineko amesema kuwa rais Felix Tshisekedi Anapenda mabadiliko Ndiyo mahana tumekuja Uvira ili kutafuta suluhisho kubwa kuusu mizozo ya kikabila ambayo inasumbuwa eneo ilo la Sud Sud ya jimbo la Kivu ya kaskazini.
Ivo pia vijiji vingi vya miji ya ndani ya Ruzizi navyo pia vinawasubiri kwa hamu kubwa kumuona kiongozi wa chama cha UDPS jimboni kivu ya kusini. http://www.fizimedia.com