Uvira: Jean Jacques Elakano atahendasha mkutano na Raiya wa Uvira

Écrit par sur juin 22, 2019

David Aluta

Wakati huu raiya wengi wakijihuliza chanzo cha ukosefu usalama ndani ya muji wa uvira jimboni kivu ya Kaskazini, hatimaye mweshimiwa mshauri wa raïsi Felix Tshisekedi,Jean Jacques Elakano amesema kuwa atakutana na raiya wa eneo hilo ili kuchambuwa hatuwa yaku tafuta Usalama na Amani yakudumu katika eneo hilo.

Jean Jacques Elakano amesema kuwa ,raiya wa tarafa na muji wa uvira wana Stahili kuhishi katika Amani ya kudumu wakati huu Raïs akiwa akichukuwa mbinu za kumaliza mizozo ya ukabila ambayo inasumbuwa eneo la Mashariki mwa Kongo.
Kwengineko huyo ameomba raiya kujumuhika wengi kunako mkutano huu ambao una malengo ya kuleta amani ndani ya Makabila yenye kuishi ndani ya eneo za uvira, Fizi, na Itombwe ndani ya tarafa ya Mwenga.
Kwao raiya wa uvira wasema kuwa wako tayari kuopokea jean Jacques Elakano kwani yeye asemaki wongo na ni yeye Ndiyo jogoo yenye kuwika mchana Kama usiku.

fizimedia.com


Les opinions du lecteur

Laisser un commentaire

Votre adresse email ne sera pas publiée. Les champs obligatoires sont indiqués avec *



En ce moment

Titre

Artiste

FiziMedia

GRATUIT
VOIR