Kongo: Mwanasheria Jean Jacques Elakano ndani ya Msafara wa Raïs , kuna nini?
Écrit par FiziMediaCongo sur juin 22, 2019
Aluta David
Katika hatuwa ya kutafuta maendeleo na amani jimboni kivu ya kusini,raïsi wa inchi ya jamuhuri ya kidemokratiya ya Kongo alimchaguwa Mwana sheria Jean Jacques Elakano moja Kati ya wanasiasa wa kongwe wa jimbo la kivu ya kusini kuwa kunaka mstari wa mbele kwenye msarafa mkubwa ambao unahenda katika mji ya uvira na fizi.
Felix Tshisekedi amesema kuona ndani ya Jean Jacques Elakano msimamo wa maendelo ya kudumu.
Jean jacques Elakano ambaye ni moja Kati ya viongozi wa chama cha UDPS na ambacho kiko leo madarakani atawasili Mjini Bukavu ambao atakuwa na kazi kubwa na viongozi kisiasa katika jimbo hilo kabla ya kujihelekeza mjini uvira ambako tayari ma elfu ya wafuasi wake raisi Felix Tshisekedi wana subiri kwa hamu kuwasili kwa kinara huyo mwenye kupigania uwongozi bora na demokratiya.
Viongozi wengi piya wamesema kusubiri kusikiya habari na salamu zake raisi wa inchi toka jean Jacques Elakano ambaye anajulikana kwa jina la jogoo.