Goma: Mwana Bunge Hope Sabini ahomba raisi Felix Tshisekedi kuweza kutimiza ahadi yake kuusu watoto kusoma bure.
Écrit par FiziMediaCongo sur septembre 19, 2019
Enoch David

Hope Sabini ni moja Kati ya wachaguliwa vijana ndani ya inchi ya jamuhuri ya kidemokratiya ya kongo na jimboni kivu ya kaskazini.
Katika maojinao ya pamoja na http://www.fizimedia.com, mwana bunge Hope Sabini amesema kuwa, raisi Felix tshisekedi amafanya Jambo nzuri kuanzisha masomo ya msingi kwa bure,bali swala kubwa ni kwamba, tarafa la rutshuru ambomo ali chaguliwa ni mfano bora ambao raisi angali pashwa hanziya.
Mchaguliwa Huyo wa tarafa la rutshuru ndani ya la bwito ndani ya Usultani wa Bwito amesema kuwa, eneo hilo limekuwa shamba la Vita Kati ya makundi ya wahasi, na hivo masomo mengi ya me haribiwa na Vita, na sio sahihi kuhanzisha masomo wakati huu watoto wengi wana baki inje bila kwenda mashuleni,ivo serekali ya inchi ingelipashwa hanza na ujenzi wa masomo ili kurusu watoto wahanze nao pia kusoma.
Kwengineko mwana bunge Huyo amaomba raisi Felix tshisekedi kuweza kutimiza ahadi hiyo na aweze kutowa neno lake kuusu kulipwa kwa walimu wakati huu wazazi wengi wanabaki ndani ya woga kuusu kulipa pesa za masomo kwa watoto.