TANZANIA: AKAMATWA KWA KUIBA MTOTO.
Écrit par FiziMediaCongo sur septembre 9, 2019
Enoch David
Jeshi la polisi mkoa wa mbeya nchini Tanzania linamshikilia mwanamke mmoja aitwae Jesca Wilson Bukuku mwenye umri wa miaka 25 mkaazi wa mtaa wa Kagera,mama John jijini Mbeya akiwa na Mtoto Ireth Ismail mwenye umri wa miezi misita akiwa hai.
Awali Agosti 29 mwaka huu mama mzazi wa mtoto huyo aitwae Élisabeth Mgina mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni mjasiriamali aliripoti kuibwa kwa mtoto wake na mwanamke asiyefahamika.
Baada ya mwanamke huho kufika sehemu yake ya biashara kama mteja kwa lengo la kununua vitunguu,lakini mtuhumiwa alidai Hana hela jivyo waende pamoja nyumbani kwake akampe hela kiasi cha shilingi elfu moja.
Anaendelea kueleza kuwa baada ya kuongozana pamoja wakiwa njiani mtuhumiwa aliomba amsaidie kumbena mtoto huyo na baadae alifika kwene nyumba aliodai ni nyumbani kwake na kuomba amsubiri kisha kutoroka na mtoto huyo.